JIZATITI KATIKA HISABATI

Sh15,000

NA HAMZA F. NAPUNDA

JIZATITI KATIKA HISABATI ni kitabu kilichoandaliwa mahususi kwa wanafunzi wa darasa la V, VI, na VII, pamoja na walimu wanaofundisha madarasa hayo. Aidha, kitabu hiki pia kinafaa sana kwa wazazi na walezi wenye tabia ya kufuatilia na kuwasaidia watoto wao kitaaluma.

JIZATITI KATIKA HISABATI Kimetungwa kwa kuzingatia mtaala mpya wa Hisabati Tanzania. Kitabu hiki kimetungwa ili kiwe msaada kwa walimu na wanafunzi wa shule za msingi, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipata ugumu katika ufundishaji wa somo la Hisabati; hali ambayo imepelekea walimu na wanafunzi kukosa ari ya kufundisha ua kujifunza somo la Hisabati.

Kitabu hiki kina mazoezi ya kutosha ambayo yametungwa kutokana na mada ndogo na madhumuni mahususi na hivyo kuwawezesha walimu kutoa mazoezi mengi na wanafunzi kufanya mazoezi hayo kwa kila mada ndogo na madhumuni maalum. Pia maumbo na michoro yote vimechorwa kwa ustadi mkubwa ili kurahisisha zoezi zima la kujjifunza na ufundishaji. Majibu ya maswali yote katika kitabu hiki yamepitiwa na kuhakikiwa kwa umakini wa hali ya juu.

Kitabu hiki cha JIZATITI KATIKA HISABATI ambacho kila mwanafunzi na kila mwalimu anatakiwa kuwa nacho kikitumika ipasavyo:

  • Kitamwezesha mwanafunzi kufanya kwa ufanisi majaribio na mitihani mbalimbali ya Hisabati na hatimaye kuweza kufaulu vizuri mtihani wa taifa wa kumaliza elimu ya msingi.
  • Kitamwezesha mwalimu kumudu kufundisha somo la Hisabati kwa ufanisi zaidi.
  • Kitamwezesha mwanafunzi kuongeza ari ya kujifunza somo la Hisabati.
  • Kitaboresha ufundishaji wa mwalimu.
  • Kitawawezesha walimu na wanafunzi kupunguza muda wa kusoma vitabu tofauti kwa ajili ya kuandaa somo ama kujifunza.

 

Description

JIZATITI KATIKA HISABATI KWA WANAFUNZI WA DARASA LA V, VI na VII, PAMOJA NA WALIMU WANOFUNDISHA MADARASA HAYO.

ISBN: 978 9987 9902 0 7

Mwandishi: Hamza F. Napunda

 

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “JIZATITI KATIKA HISABATI”

Your email address will not be published. Required fields are marked *