JIZATITI KATIKA KSWAHILI

Sh15,000

Na Hamza F. Napunda

JIZATITI KATIKA KISWAHILI: Ni kitabu kilichoandaliwa mahsusi kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la V, VI, na VII, pamoja na walimu wanaofundisha madarasa hayo. Aidha kitabu hiki pia kinafaa sana kwa wazazi na walezi wenye tabia ya kufuatilia na kuwasaidia watoto wao kitaaluma.

JIZATITI KATIKA KISWAHILI: Kimetungwa kwa kuzingatia mtaala mpya wa somo la Kiswahili Tanzania. Kitabu hiki kimeandaliwa ili kiwe msaada kwa walimu na wanafunzi wa shule za msingi, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipata ugumu katika ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Kiswahili; hali ambayo imepelekea wanafunzi kupata matokeo yasiyoridhisha katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi, kinyume kabisa na matarajio ya wengi.

Description

Maelezo

Kitabu hiki cha JIZATITI KATIKA KISWAHILI ambacho kila mwanafunzi na kila mwalimu anatakiwa kuwa nacho kikitumika ipasavyo:

  • Kitamwezesha mwanafunzi kufanya kwa ufanisi majaribio na mitihani mbalimbali ya somo la Kiswahili na hatimaye kuweza kufaulu vizuri mtihani wa Taifa wa kumaliza elimu ya msingi.
  • Kitamsaidia mwalimu kuweza kufundisha somo la Kiswahili kwa ufanisi zaidi.
  • Kitamwezesha mwanafunzi kuongeza ari ya kujifunza somo la Kiswahili na hatimaye kuweza kumudu vyema lugha yetu adhimu ya Taifa
  • Kitaboresha ufundishaji wa mwalimu.
  • Kitawawezesha walimu na wanafunzi kupunguza muda wa kusoma vitabu vingi tofauti tofauti kwa ajili ya kuandaa somo ama kujifunza.

Mbali na kitabu cha JIZATITI KATIKA Kiswahili mwandishi huyu pia kaandika vitabu vifuatavyo, vinavyofanya vizuri katika soko la vitabu.

Mwandishi: Hamza F. Napunda
Mchapishaji: Vanedi Books Limited
Lugha:Kiswahili
ISBN: 978 9976 5465 6 9
Toleo la : Kwanza
Kimechapishwa mwaka: 2019

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “JIZATITI KATIKA KSWAHILI”

Your email address will not be published. Required fields are marked *