JIZATITI KATIKA SAYANSI

Sh15,000

JIZATITI KATIKA SAYANSI KWA WANAFUNZI WA DARASA LA V, VI NA VII NA HAMZA F. NAPUNDA

JIZATITI KATIKA SAYANSI ni kitabu kilichoandaliwa mahususi kwa wanafunzi wa darasa la V, VI, na VII, pamoja na walimu wanaofundisha madarasa hayo. Aidha, kitabu hiki pia kinafaa sana kwa wazazi na walezi wenye tabia ya kufuatilia na kuwasaidia watoto wao kitaaluma.

JIZATITI KATIKA SAYANSI Kimetungwa kwa kuzingatia mtaala mpya wa Sayansi Tanzania. Kitabu hiki kimetungwa ili kiwe msaada kwa walimu na wanafunzi wa shule za msingi, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipata ugumu katika ufundishaji wa somo la Sayansi; hali ambayo imepelekea walimu na wanafunzi kukosa ari ya kujifunza somo hili muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu.

Kitabu hiki kina mazoezi ya kutosha ambayo yametungwa kutokana na mada ndogo na madhumuni mahususi na hivyo kuwawezesha walimu kutoa mazoezi mengi na wanafunzi kufanya mazoezi hayo kwa kila mada ndogo na madhumuni maalum. Pia maumbo na michoro yote vimechorwa kwa ustadi mkubwa ili kurahisisha zoezi zima la kujjifunza na ufundishaji. 

Kitabu hiki cha JIZATITI KATIKA SAYANSI ambacho kila mwanafunzi na kila mwalimu anatakiwa kuwa nacho kikitumika ipasavyo:

  • Kitamwezesha mwanafunzi kufanya kwa ufanisi majaribio na mitihani mbalimbali ya Sayansi na hatimaye kuweza kufaulu vizuri mtihani wa taifa wa kumaliza elimu ya msingi.
  • Kitamwezesha mwalimu kumudu kufundisha somo la Sayansi kwa ufanisi zaidi.
  • Kitamwezesha mwanafunzi kuongeza ari ya kujifunza somo la Sayansi.
  • Kitaboresha ufundishaji wa mwalimu.
  • Kitawawezesha walimu na wanafunzi kupunguza muda wa kusoma vitabu tofauti kwa ajili ya kuandaa somo ama kujifunza.

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “JIZATITI KATIKA SAYANSI”

Your email address will not be published. Required fields are marked *